Jinsi Ya Kujizuia Kutofanya Mapenzi Katika Mahusiano Mapya
Kuingia katika mahusiano mapya ya kimapenzi huwa ni furaha na kuchanganya pia. Unaingiwa na hisia ambazo hujawahi kuwa nazo na pia kupenda kwa dhati. Mpenzi wako anakufurahisha na wewe pia unamfurahusha. Lakini inaweza kutokezea sitofahamu wakati ambapo wewe hutaki ama hujiskii kufanya mapenzi lakini yeye akawa na hamu ya kufanya tendo hilo. Sababu zozote zile uko nazo, una haki ya kujizuia kutofanya tendo la ngono mpaka ile siku ambayo utajiskia kuwa umefikia siku yako. Mwili ni wako na maamuzi ni yako. So utafanyaje umzuie mpenzi wako kutofanya ngono na wewe? Mambo ya kufanya kumzui mpenzi wako kutofanya mapenzi nawe 1. Usilale kwake Iwapo hautaki kufanya mapenzi na mpenzi wako, basi ni vizuri usijiingize katika hali ambazo zitachangia nyinyi wawili kuingiwa na hamu ya mapenzi. Iwapo umetoka deti na mpenzi wako, usijaribu kumsindikiza hadi kwake ama kuenda njia moja. Pia hutakiwi kuwa unazunguka sehemu ambazo mpenzi wako anaishi wakati kama huo kwa sababu inaweza kuchangia pakub...