Mfanyabiashara Auawa gesti Kwa Kuchomwa Kisu
Mfanyabiashara wa mazao, Eliusta Peter(40), amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni akiwa katika nyumba ya kulala wageni wilayani Kilombero. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea Aprili 22 baada ya wahudumu wa nyumba ya wageni ya Sayari kubaini maiti katika chumba namba mbili. Inadawa Aprili 20 mwanamke huyo akiwa na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi, walifika kwenye nyumba hiyo na kuchukua chumba kimoja wakisema wao ni wafanyabiashara wa mazao. “Mwili wa marehemu uligundulika ukiwa kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Sayari chumba namba mbili saa 11 jioni na ulipochunguzwa ikagundulika kuwa kifo kilisababishwa maumivu ya jereha,” alisema Matei. Mwanamke huyo alikuwa na jeraha kushoto mwa bega lake lililotokana na kuchomwa na kitu che...