Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Yakataa Kuipokea Taarifa ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Taarifa ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) iliyowasilishwa jana kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imekataliwa baada ya kubainika upungufu, ukiwamo udhaifu wa Sera ya Uwekezaji na kiasi cha fedha kilichowekezwa katika miradi iliyopita. Uamuzi huo umekuja wiki moja baada ya kamati hiyo kuagiza kusimamishwa miradi yote mipya inayotarajiwa kutekelezwa na NSSF hadi Serikali itakapopitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kujiridhisha na utendaji wa mfuko huo. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamed Mchengulwa alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara katika ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ambapo baada ya kupokea ripoti ya SSRA, alisema: “Kamati inaagiza kwamba SSRA isimamie miradi yote mipya inayotarajiwa kutekelezwa hivi sasa isimame haraka, ili iweze kujiridhisha na hesabu ambazo zimefanyika.” Akizungumza baada ya kikao kati ya kamati hiyo na NSSF jana, Mchengulwa alisema mbali ya mfuko huo ku...