Mamlaka ya Bandari-TPA Yataja Sababu Iliyosababisha Mizigo Bandarini Dar es Salaam Kupungua
Siku moja baada ya serikali kuziagiza mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi wa kina ili kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Alois Matei, leo amejitokeza mbele ya waandishi wa habari ili kutaja chanzo cha mizigo kupungua bandarini. Agizo la kuzitaka mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi huo lilitolewa juzi Bungeni April 30 na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dr. Philip Mpango . Dr Mpango alisema katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu kontena zilizopelekwa nchini Congo zilishuka kutoka 5,529 hadi 4,092, wakati yale yaliyokuwa yakipelekwa nchini Malawi yalishuka kutoka kontena 337 hadi 265, huku yale ya Zambia yakishuka kutoka 6,859 hadi kufikia 4,448, hivyo akaziagiz...