Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Polisi Apigwa Jiwe Kichwani

Wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki na Kampuni ya Vinywaji ya Pepsi (SBC) Wagoma.......Mabomu Yatumika Kuwatuliza, Polisi Apigwa Jiwe Kichwani

Picha
Miezi michache baada ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kukwaruzana na Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea chanzo kikiwa ni mgogoro wa Kiwanda cha Urafiki na kupelekana mahakamani, jana mabomu yalirindima kiwandani hapo wakati wafanyakazi wakiendeleza madai ya malimbikizo ya mishahara.  Awali, viongozi hao walifikishana mahakamani baada ya Kubenea kudaiwa kumtukana Makonda ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wakitatua moja ya migomo ya wafanyakazi hao.  Kubenea alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu nje na kutotakiwa kutoa lugha ya matusi kama alivyofanya kwa mkuu huyo, lakini madai ya wafanyakazi wa Urafiki bado hayajapata suluhu.  Katika vurugu hizo zilizoanza jana asubuhi askari mmoja alipigwa jiwe kichwani huku wafanyakazi watatu wakizirai.  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema vurugu hizo zilianza baada ya wafanyakazi hao kutoelewana.  “Waliokuwa tayari kuendelea na kazi waliz...