Saudia yatishia kutumia nguvu za kijeshi kumuondoa Rais wa Syria madarakani
Saudi Arabia imerudia kauli zake za kifedhuli za kuingilia masuala ya ndani ya Syria kwa kutishia kwamba endapo mazungumzo ya kisiasa ya kutatua mgogoro wa nchi hiyo yatafeli itatumia nguvu za kijeshi dhidi ya Rais Bashar al-Asaad. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Adel al-Jubeir baada ya mazungumzo ya Kundi la Kimataifa la Kuiunga Mkono Syria (ISSG) yaliyofanyika jana mjini Vienna, Austria. Al-Jubeir amedai kuwa anavyoamini ilipasa muda mrefu nyuma kufikiria mpango mbadala, ambao unatilia nguvu kuwapatia misaada zaidi ya kijeshi wapinzani wa Rais Bashar al-Assad wa Syria. Utawala wa Aal Saudi ni miongoni wa waungaji mkono wakubwa wa mpango wa kumwondoa madarakani Rais Assad na ni mfadhili mkubwa wa fedha na silaha kwa makundi yanayobeba silaha yanayotaka kuiangusha serikali halali ya Syria. Duru ya mazungmzo yasiyo ya ana kwa ana ya kusaka amani baina ya serikali na wapinzani wa Syria yanayofanyika kwa usuluhishi wa Umoja wa Mataifa, yaliyoanza tarehe 13 y...