YANGA YAPANGIWA WAANGOLA KOMBE LA SHIRIKISHO
CAIRO,MISRI Klabu ya Yanga ya Tanzania imepangwa kukutana na klabu ya Sagrada Esperanca Angola katika hatua ya mtoano (16 bora) ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga itaanzia nyumbani kati ya tarehe 6 hadi 8 mwezi Mei, na marudiano itakuwa nchini Angola kati ya tarehe 17 na 18 mwezi huohuo. Yanga imefikia hatua hiyo baada ya kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Mabingwa Barani Afrika na Al Ahly baada ya kufungwa 2-1 katika mchezo wa marudiano uliopigwa jana nchini Misri. Jumla ya timu 8 zilizotolewa katika michuano hiyo pamoja na Yanga zimeshushwa katika michuano ya Kombe la Shirikisho na kukutana na timu nyingine 8 zilizofuzu kutoka raundi ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho. Shirikisho la Soka Barani Afrika limeendesha droo muda mfupi uliopita na matokeo ya droo hiyo ni kama ifuatavyo. Michezo yote ya kwanza itachezwa kati ya tarehe 6 na 8 mwezi Mei na marudiano ni kati ya tarehe 17 na 18 mwezi Mei. Kati ya timu hizo 16, timu nane zilizofuzu 8 bora kupitia mich...