Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SIMEONE

SIMEONE, KOCHA MWANAHARAKATI NA SHUJAA WA ATLETICO MWENYE NDOTO KALI ZA UEFA

Picha
Na Mahmoud Rajab Diego Simeone ni mpambanaji. Kamwe hilo huwezi kupinga na mara zote yeye kama kocha na wachezaji wake hufanya hivyo kwa maslahi ya timu kutokana na timu kutokuwa na bajeti ya kununua wachezaji kwa pesa nyingi. Kuna wakati aliwahi kuhojiwa juu ya aina ya uchezaji wake kwamba kwanini uko ‘too physical’? alichokisema ni kwamba: ‘Wazazi wangu waliniambia nicheze mpira kama mwanajeshi”. Diego Simeone ni mtu ambaye anaamini kila mchezaji kwenye timu yake apambane mpaka tone la mwisho. Falsafa yake ni kwamba huwa kama mchezaji hataki kujitoa kwa asilimia zote kwa ajili ya timu, basi hawezi kufanya naye kazi. “Nawashukuru sana wazazi waliowazaa wachezaji hawa”, hiyo ni kauli ya Simeone aliyoitoa wakati ameshinda game ya Champions League dhidi ya Chelsea mwaka 2014. Ni maneno yaliyolenga kuwapa morali wachezaji wake na hatimaye kutinga fainali na kufungwa na Real Madrid. Matokeo yale yalimuumiza kutokana na kufungwa kusikotarajiwa baada y...