Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Vikosi maalum vya Ufaransa vyaingia Benghazi

Vikosi maalum vya Ufaransa vyaingia Benghazi, Libya

Vikosi maalumu vya Ufaransa vimewasili Benghazi, Libya kumuunga mkono Brigedia Jenerali Khalifa Haftar.Imedokezwa kuwa vikosi hivyo,viko katika Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Benina mashariki mwa Benghazi ambayo ni ngome muhimu zaidi ya askari watiifu kwa Haftar. Haijabainika idadi ya wanajeshi wa Ufaransa walioingia mjini humo. Siku ya Jumapili Haftar alitangaza kuwa askari wake wamechukua udhibiti wa mji wa Ajdabia na Bandari ya AL Muraisah. Maeneo hayo yalikuwa yanashikiliwa na wanamgambo na magaidi wakufurishaji. Vikosi vya Jeshi la Libya chini ya usimamizi wa Haftar vinaiunga mkono serikali ya Libya yenye makao yake mjini Tobruk mashariki mwa nchi hiyo ambayo inatambuliwa kimataifa.Wakati huo huo Bunge la Libya limeakhirisha upigaji kura kuhusu serikali mpya ya umoja wa kitaifa kutokana na kukosekana idadi inayohitajika ya wabaunge wanopiga kura. Spika wa Bunge ameakhirisha zoezi hilo hadi wiki ijayo kutokana na kuwa kulikuwa na wabunge chini ya 89.Serikali mpya ya Libya ilitangaz...