Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SAKATA LA KITWANGA KULEWA BUNGENI CCM WATOA TAMKO

SAKATA LA KITWANGA KULEWA BUNGENI CCM WATOA TAMKO

Picha
CCM imesema kitendo cha Rais John Magufuli kumvua uwaziri Charles Kitwanga kutokana na kuingia bungeni akiwa amelewa, kimedhihirisha kuwa bado kuna baadhi ya watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma, lakini hakitachukua hatua kwa kuwa ameshaadhibiwa. Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka jana alisema kitendo cha Kitwanga kuingia bungeni akiwa amelewa kimewapa fundisho na sasa wanajua kuwa kuna baadhi ya watumishi waliopewa dhamana na chama hicho, lakini wanakiuka miiko ya maadili ya utumishi wa umma, jambo ambalo ni kinyume na taratibu zao. Sendeka alisema licha ya kwamba Rais Magufuli amechukua hatua juu ya hilo na kutoa adhabu, CCM itaendelea kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya wanasiasa waliopewa dhamana na chama hicho. “Hatutasita kuchukua hatua endapo tutabaini kuna kada anayekiuka maadili ya viongozi wa umma,” alisema Sendeka. Alisema CCM inampongeza Rais Magufuli kwa uamuzi aliochukua dhidi ya Kitwanga kwa kuwa hatua hiyo imedhihirisha kauli aliyowahi k...