Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ziko Wapi Nyimbo za Wasanii wa Top 5 ya BSS?

Madam Rita, Ziko Wapi Nyimbo za Wasanii wa Top 5 ya BSS?

Picha
Bongo Star Search ni shindano pekee kwa Tanzania la kusaka vipaji kwa vijana wenye uwezo wa kuimba.  Madam Rita kupitia kampuni yake ya Benchmark Production alikuwa na malengo mazuri ya kuanzisha shindano hili ambalo watanzania tulikuwa tunaangalia mashindano kama haya katika nchi za nje tu.  Kwa mara ya kwanza shindano la BSS lilianza mwaka 2007 na lilizalisha vipaji kama, Kala Jeremiah, Baby Madaha, na aliyekuwa mshindi wa shindano hilo Jumanne Iddi ambaye kwa sasa amepotea kwenye ramani ya muziki.  Mashindano ya BSS, msimu wa nane mwaka 2015 yamesaidia kuvitambua vipaji vingi vilivyokuwa vimejificha. Washiriki watano waliofanikiwa kuingia kwenye fainali za shindano hilo ni Kayumba Juma, Nassibu Fonabo, Frida Amani, Angel Mary Kato na Kelvin Gason.  Tunakumbuka kuwa kwenye shindano hilo, Kayumba Juma alifanikiwa kushinda na kufanikiwa kupata mkwanja wa shilingi milioni 50. Moja ya ahadi zilizotoka kwenye mashindano hayo ni kuwa top five yote itakuwa chini ya ...