Algeria yapinga kutolewa tuhuma za ugaidi dhidi ya Hizbullah ya Lebanon
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Algeria Algeria imepinga kutolewa taarifa ya Mawaziri wa Mambo ya Ndani wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.Kwa mujibu wa chombo cha kuaminika katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Algeria nchi hiyo ilipinga vikali kuorodheshwa kwa harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu kama kundi la kigaidi na kuongeza kuwa kutolewa tuhuma zozote dhidi ya nchi hiyo kutokana na msimamo wake kuhusu harakati hiyo ya Kiislamu ni kuvunjiwa heshima nchi hiyo na kufanyika juhudi za kuiingiza katika migogoro ya kieneo.Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani wa nchi wanachama wa Arab League jana Jumatano lilitoa taarifa mwishoni mwa kika chake cha 33 huko Tunis mji mkuu wa Tunisia ambapo liliiorodhesha Hizbullah ya Lebanon kama mojawapo ya makundi ya kigaidi, kinyume kabisa na matakwa ya wananchi wa mataifa ya Mashariki ya Kati. Baraza hilo lilidai kuwa mapambano ya Hizbullah dhidi ya ugaidi wa Wazayuni wa Israel na utakafiri w...