Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Bajeti ya Magufuli 2016/17 Hadharani Leo....Macho na Masikio Yote Yaelekezwa Dodoma

Bajeti ya Magufuli 2016/17 Hadharani Leo....Macho na Masikio Yote Yaelekezwa Dodoma

Picha
TANZANIA kama zilivyo nchi nyingine za Afrika Mashariki, leo inawasilisha bungeni mjini Dodoma Bajeti ya Serikali ili Bunge liijadili na kuipitisha, ianze kutekelezwa katika mwaka mpya wa fedha 2016/17 unaoanza Julai mosi. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango anatarajiwa kuiwasilisha bajeti hiyo inayoelezwa kuwa na Sh trilioni saba zaidi ya ile iliyopitishwa na Bunge hilo mwaka jana, ambayo utekelezaji wake unaishia Juni 30, 2016. Hii ni bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, ambaye ameeleza kuwa anataka kujenga Tanzania ya viwanda, ambayo nia ni kuifanya iwe na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Tofauti na bajeti ya mwaka jana ya jumla ya Sh trilioni 22.495 zilizotengwa kutoka katika vyanzo vya ndani na nje, bajeti nzima ya mwaka huu kwa mujibu wa mapendekezo ya ukomo wa bajeti hiyo yaliyowasilishwa kwenye mkutano wa wabunge wote Dar es Salaam, Aprili 6, mwaka huu ni Sh trilioni 29.539. Bajeti hiyo inayosubiriwa kwa hamu na W...