💔 Siri Nzito Ndani ya Hoteli: Kilio, Aibu na Tukio Lisilosahaulika Maishani | T MEDIA NEWS
Simu yangu ikaanza kuita, nikapiga hatua za haraka kwenda kuipokea huku nikimgonga kidogo muhudumu begani. Kitendo cha kuinama na kuiokota suruali yangu iliyokuwa chini ili kutoa simu mfukoni, ghafla taulo langu likafunguka na kudondoka chini huku muhudumu akibaki ananishangaa. ENDELEA Nilibaki nimeshika butwaa, akili yangu ikiwa imechanganyikiwa kwa sekunde chache. Sikujua nianze wapi—kuokota taulo au kupokea simu. Aibu ilinipanda ghafla, lakini simu iliendelea kuita bila huruma. Muhudumu alikuwa amesimama kama sanamu. Hakusogeza hata jicho, macho yake yakiwa yameganda kunitazama. Nilijaribu kujisitiri haraka kwa kuokota taulo, huku moyo wangu ukidunda kwa kasi isiyo ya kawaida. Hatimaye niliitoa simu mfukoni na kuona ni Rahma anayepiga. Nikapokea kwa sauti ya kawaida kadiri nilivyoweza kujizuia: “Hello baby…” “Baby, umeshaletewa chakula?” Rahma aliuliza kwa sauti ya upole. “Ndio baby,” nikajibu huku bado najisitiri kwa haraka. “Ok, mimi nimeshafika kwa bibi. Nikitaka kuja huko nitaku...