YAJUE MADHARA MAKUBWA YATOKANAYO NA UTOAJI MIMBA
Utoaji wa mimba limekuwa jambo sugu na linalokuwa kwa kasi sana hasa kwa wasichana bila kufahamu madhara yake.sababu kuu ya kutoa mimba ni kupata ujauzito bila kuwa na mpango maalumu na mwenza wake, wasichana wengi Hubeba mimba shuleni. jambo lakushangaza Imekuwa la kawaida sana kwa watu walio kwenye mahusiano, kwani wamekuwa wakipuuzia matumizi ya kinga kwa kujidanganya utamu wa mapenzi kupungua,wakati huohuo wakijua kuna madhara mengi sana kufanya Tendo hilo bila kuzingazitia matokeo baada ya uzembe huo… Madhara yanayoambatana na utoaji mimba ni vifo, kupoteza damu nyingi, kifafa cha uzazi na maambukizi hatarishi katika mfuko wa uzazi au mirija ya uzazi. Haya yote yanaambatana na homa kali na maumivu makali, kutunga usaha kwenye kizazi na kulazimika kufanyiwa upasuaji wa dharura au haraka kitaalamu; kikubwa mara nyingi ni kifo. Mhusika kama akipona kutokana na athari ya kuichokonoa mimba visivyo au kwa nguvu sana, wakati mwingine husababisha uharibifu wa ...