JINSI YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA KUHARA KWA WATOTO
Katika magonjwa ambayo huwasumbua watoto mara kwa mara ni ugonjwa wa kuhara, lakini habari njema ni kuwa ugonjwa huu humalizika ndani ya siku chache mtoto anapohudumiwa vyema. Lakini pamoja na hayo ni vyema kujua jinsi ya kumsaidia mtoto anayekabiliana na ugonjwa huu na jinsi ya kuwakinga wale wasio na ugonjwa. Ni nini kinachosababisha ugonjwa wa kuhara? Kuhara ni ugonjwa ambao husababishwa kwa kiasi kikubwa na aina ya virusi, lakini pia yaweza kua bacteria au vimelea vinginevyo vya magonjwa. Mtoto(mgonjwa) hupata choo mara nyingi ambacho ni majimaji. Aina ya vijimelea vinavyosababisha kuhara kwa watoto hutegemea eneo la kijiografia kulingana na viwango vya usafi wa mazingira, hali ya kiuchumi na usafi wa mwili. Kwa mfano nchi zinazoendelea ambapo hali ya usafi wa mazingira ni duni na maeneo ambayo kinyesi cha binadamu hutumika kama mbolea, hukabiliana na milipuko ya magonjwa ya kuhara mara kwa mara kwa sababu taka hizi zitokanazo na binadamu ni rahisi kuingia katika vyakula n...