HIZI NDIO TABIA TISA ZINAZOSABABISHA VIJANA WA SIKU HIZI KUZEEKA HARAKA
sasa hivi ukifanya utafiti mdogo tu hakuna mtu anayependa kuzeeka, iwe mwanaume au mwanamke lakini pia uzee ni kitu ambacho kinaleta sana msongo wa mawazo kwani ukiangalia picha zako kipindi una miaka 18 na sasa hivi una miaka 35 au 40 tayari umeshaona mabadiliko makubwa sana kwenye mwili yako lakini pia hofu ya kifo kwani unajua kinachofuata baada ya uzee ni kifo tu. japokua uzee haukwepeki leo hii kuna watu wana miaka 20 lakini wanaonekana wana miaka 30. hii ni dalili mbaya sana na huambatana na tabia zifuatazo mara nyingi. kutofanya mazoezi kabisa; kiasili sisi binadamu ni wavivu, yaani watu wote wanaofanyakazi ni kwasababu wanajua wasipofanya kazi watalala njaa. lakini vizuri haviji bure hata utajiri unataka mateso kuupata. maana yangu ni kwamba mazoezi ndio yanafanya ngozi zetu na miili yetu iendelee kua kakamavu lakini pia huzuia uzito ambao ndio moja ya vyanzo vikuu vya unene.binadamu yeyote anatakiwa afanye mazoezi angalau dakika 20 kwa siku. usisingizie kazi au kwamba ...