Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Hakuna Wa Kukusaidia Katika Maisha yako

Usipojiandaa Kwa Mabadiliko Haya, Hakuna Wa Kukusaidia Katika Maisha yako

Picha
Dunia imekuwa ndogo sana,bila kujali utaiita kitu gani. Kama utaita utandawazi, sayansi na teknolojia, demokrasia zaidi, uchumi wa soko, teknolojia ya habari au chochote, ukweli unabaki kuwa huo. Ni jambo la kusikitisha sana kuona wasomi na wanasiasa ambao kwa bahati mbaya naweza kusema hawana jipya sana kwa jamii, wakilaumu serikali kwenye suala la utandawazi.   Nijuavyo mimi, mabadiliko ya kijamii hayawezi kuzuiwa na mtu, hata kama angekuwa na uwezo wa kiwango gani, labda anachoweza ni kufanya uharibifu wa kuwafuja watu na matokeo yake ya kawaida hayapendezi sana. Hakuna mtu ambaye angeweza kuzuia mfumo wa maisha holela ya binadamu wa awali ambapo mali ilikuwa ni kiwango cha nguvu za mwili alizokuwa nazo binadamu. Yule aliyeweza kuua Tandala kwa jiwe ndiye aliyekuwa akiheshimiwa na kufikia mafanikio kirahisi. Hakuna ambaye angeweza kuzuia mfumo huo kuupisha ule wa uchifu, ambapo mwenye kauli na uwezo wa karibu kabisa kufanikiwa alikuwa ni mtu yeyote kutoka ukoo wa kichifu. Ha...