Nape Ataja Majipu Manne Katika Sanaa Nchini,aahidi Kuyatumbua
Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na michezo nchini,Nape Nnauye ametaja mambo manne ambayo ni vikwazo ndani ya sekta ya sanaa ya filamu nchini na kuyaita kwamba ni majipu huku akisisistiza kwamba serikali itakwenda kutunga sera ya sekta hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17. Nape,aliyataja mambo hayo na kuyafananisha na majipu kuwa ni uporaji wa kazi za wasanii nchini,ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii nchini,usimamizi mbovu wa bodi ya filamu nchini sanjari na tatizo la mfumo mbovu wa usambazaji wa kazi za wasanii nchini. Akizindua tamasha la filamu la Tanzanite International Film Festival(TIFF) jijini Arusha juzi ambao ulihudhuriwa na wasanii maarufu wa filamu nchini waziri huyo alisema kwamba jipu la kwanza ambalo atakwenda kulitumbua ni uporaji wa kazi za wasanii nchini. “Jipu la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka 2016/17 ni uporaji wa kazi za wasanii nchini wengi wananyonywa jasho lao”alisema Nape Hatahivyo,alisema kw...