Waziri Ataka Wakurugenzi NHC Washindanishwe
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula, ametaka wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika mikoa yote washindanishwe kujua utendaji kazi wao. Waziri Mabula, alitoa kauli hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa shirika hilo kilichokuwa kikijadili mipango na makisio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/17 kabla ya kuwasilishwa bungeni. Alisema hatua hiyo itasaidia kutambua wakurugenzi ambao wanasubiri kubebwa na wenzao kwa kushindwa kufanya kazi kwa weledi. Alisema ujenzi na ununuzi wa nyumba unahitaji fedha nyingi, wananchi hununua nyumba kupitia mikopo kutoka benki. "Serikali inatambua umuhimu wa taasisi za fedha katika kusaidia ukuaji wa sekta ya nyumba jambo ambalo hufanywa duniani kote, " alisema. Alisema Serikali inatambua bado kuna changamoto ya riba kubwa ya mikopo ya nyumba...