Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangalla Yajitolea Kumsomesha Getrude Clement
Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa kizazi cha miaka ijayo, Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla iliyoanzishwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla imejitolea kumlipia ada Getrude Clement kwa masomo yake ya kidato cha tano na sita. Uamuzi huo wa kumsomesha Getrude umekuja baada ya jana kukaribishwa kuongea kwenye kikao cha wabunge watetezi wa haki za watoto ambapo Getrude alipata nafasi ya kutoa historia yake ambayo iliwatoa baadhi ya wabunge machozi. Getrude aliwaeleza wabunge historia yake na hali yake ya kimaisha na kusema kuwa baba yake ni kinyozi na mama yake anafanya biashara ndogo ndogo za nyanya na vitunguu lakini bado amekuwa akijtuma katika masomo yake ambapo kwa sasa yupo kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Mnarani, Mwanza. Baada ya kusema hivyo, ndipo Dkt. Kigwangalla aliamua kujitolea kumsaidia mtoto huyo ili aweze kujiendeleza zaidi kielimu na kufikia malengo yake na zaidi akiahidi kums...