Samatta vs Karelis Nikolous: Hivi ndivyo namba 77 vs 7 zinavyoshindana nchini Ubeligiji
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta bado hajakuwa na wakati mgumu na Timu yake ya KRC GENK inayoshiriki ligi kuu Ubeligiji Pro League kama wanavyodhani watu wengi. Samatta anatokea benchi kwenye mechi zote alizocheza hadi sasa kuchukua nafasi ya mshambuliaji raia wa ugiriki Karelis Nikolous. Kuonesha kwamba yupo vizuri, wikiendi iliyopita Samatta alifanikiwa kufunga goli lake la kwanza klabuni hapo walipokutana na vinara wa ligi hiyo Club Brugge. Makala hii inakuletea takwimu muhimu kuhusu Mbwana Samatta, jezi namba 77 dhidi ya Mgiriki Karelis Nikolaos namba 7 ambaye mara kadhaa anapotoka Samatta anaingia Magoli (1 vs 4) Mbwana Samatta hadi sasa amefanikiwa kupachika wavuni goli 1, wakati Mgiriki Nikolous amefunga mara 4. Samatta alifunga goli lake kwenye mchezo dhidi ya Club Brugge dakika 81 baada ya kutokea benchi dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Karelis Nikolous. Mechi (4 vs 7) Mbwana amecheza michezo mine (4) akiwa na KRC GENK, amba...