FIRST ELEVEN YA WACHEZAJI WA EPL WATAOKOSEKANA EURO 2016
Na Mahmoud Rajab Dejan Lovren, Vincent Kompany, Morgan Schneiderlin na Diego Costa wote kwa pamoja hawatoonekana katika michunao ya Euro mwaka huu nchini Ufaransa. Wachezaji wengi wenye majina makubwa wanaocheza ligi ya England watakuwa na timu zao kwenye EURO mwaka huu. Mataifa yote 24 yakayokuwa yakiwania ubingwa huo, yamechagua vikosi vyao kwa ajili ya michuano hiyo, ambayo itaanza June 10. Hata hivyo , kuna baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa ambao watakosekana katika EURO ya mwaka huu baada ya ama kutokuchaguliwa kutokana na majeraha au viwango vyao kutowaridhisha makocha wao. Mtandao wa Sky Sports umekuja na first eleven ya wachezaji hao watakaokosa EURO mwaka huu. Mlinda lango: Rob Elliot (Jamhuri ya Ireland) Rob Elliot alipata majeraha wakati wa mchezo wa kirafiki. Kipa huyu wa Newcastle United atakosa mashindano hayo kutokana na kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Slovakia mwezi March mwaka huu. Beki wa kulia: Kurt Zouma (Ufaransa) Kurt Zouma atakosa kuto...