Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Magufuli Kujaza Vijana Serikalini....Adai Wazee Ndo Wameihairibu Hii Nchi

Magufuli Kujaza Vijana Serikalini....Adai Wazee Ndo Wameihairibu Hii Nchi

Picha
Kuanzia sasa wateule wengi wa Rais John Magufuli serikalini watakuwa vijana kwa kuwa amegundua wengi hawapendi rushwa, amesema. Aidha, Rais Magufuli amesema anafahamu kwamba vijana hawapendwi lakini amegundua ndio wachapakazi ambao watasaidia kulipeleka taifa katika maendeleo anayoyatamani.    Rais Magufuli alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano wa makandarasi wa mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Dodoma, jijini.    “Nimegundua vijana wengi hawapendi rushwa, hivyo nitaongeza vijana kila nikiteua kwa kuwa niliowaweka naona matunda ya kazi zao,"  alisema na kuongeza kuwa: “Najua watu wanawachukia sana ila nitawaongeza.    “Palipo na vijana nimeona mambo yanaenda na kuna mabadiliko. Wazee ndio tumelifikisha taifa hili hapa. Hakuna asiyejua kuwa Tanzania ilichakaa kila mahala.”    Tangu aingie Ikulu Novemba 5, mwaka jana, Rais Magufuli amejipambanua kama mwenye kupiga vita wizi, rushwa, ufisadi, ukwepaji ...