Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kitwanga Ang'aka Jina Lake Kutajwa

Agizo la Rais Magufuli Laanza kutekelezwa ......Waziri Mahiga arudisha Fomu , Kitwanga Ang'aka Jina Lake Kutajwa

Picha
Baada ya waziri mkuu kutaja majina ya mawaziri wanne na naibu waziri mmoja ambao hawajarudhisha fomu za Sekretariati ya maadili ya umma na kutakiwa wawe wamerejesha fomu hizo kabla ya  saa kumi na mbili jioni ijumaa ya leo mpaka sasa ni waziri mmoja aliyetii agizo hilo Aliyerudisha fomu hizo ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga ambapo amekiri kuwa ni kweli alikuwa hajarudisha fomu hizo kutokana na majukumu ya kazi yaliyokuwa yamembana Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga yeye  ameshangaa jina lake kutajwa wakati tayari ameshazirudisha fomu hizo. Amesema hivi sasa  ameelekea ofisi za Sektretariati ya maadili kuwasilisha malalamiko yake Naibu Waziri wa  Nchi (OMR – Mazingira), Bw. Luhaga Mpina yeye amesema kuwa atawahisha kurudisha fomu hizo kabla ya saa kumi na mbili jioni.