JWTZ Yajitosa Mauaji Ya Watu 8 Tanga.......Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange Atangaza Msako usiku na Mchana
SERIKALI imetuma kikosi maalumu cha ulinzi, kikiongozwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuwasaka watu wanaodaiwa kuwa majambazi ambao wanaendesha mauaji ya kinyama mkoani Tanga. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya watu wanane kuuawa kinyama kwa kuchinjwa juzi usiku katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Manispaa ya Tanga. Habari za uhakika ambazo tulizipata jana, zinasema tayari vikosi hivyo vimeanza operesheni kali katika mapango ya Amboni ambayo yanadaiwa kuwa maficho ya watu hao. Akitoa salamu za rambirambi wakati wa mazishi ya marehemu wanne kati ya wanane waliozikwa Kibatini jana, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema vyombo vya dola vitahakikisha watu wote waliohusika katika mauaji hayo wanatiwa mbaroni. “Ndugu zangu nawapeni pole kutokana na kuondokewa na wapendwa wetu… naomba kuwahakikisha sisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola tutahakikisha tunawatia nguvuni watu wote waliohusik...