CCM YAIGALAGAZA CHADEMA ARUSHA MJINI
ARUSHA CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha Mjini kimepata ushindi wa viti vitano dhidi ya vitatu vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwenye uchaguzi wa wenyeviti wa serikali ya mtaa. Uchaguzi huo ulifanyika juzi kutokana na wenyeiti wa mitaa tisa, kuhamia vyama mbalimbali vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Katibu wa CCM wilaya ya Arusha Mjini, Feruzi Bano alisema ushindi huo unatokana na kasi ya Rais John Magufuli ya utumbuaji majipu, ambayo imewakuna wananchi wengi na kuanza kupenda chama hicho tawala. Bano alitaja mitaa ambayo CCM imeshinda ni mtaa wa Olamuriaki kata ya Sombetini na mtaa wa Shangarau kaya ya Moivaro, ambapo katika mitaa yote hiyo, CCM imepita bila kupingwa baada ya Chadema kushindwa kusimamisha wagombea. Mitaa mingine ambayo CCM imeshinda ni mtaa wa Makao Mapya kata ya Sinoni, mtaa wa Bondeni kata ya Kati na mtaa wa Kilimaji kata ya Moshono. Kwa upande wa wajumbe wa serika...