Kamanda Kova Ambwaga Tena Nzowa Mahakamani
Mahakama ya Rufaa Tanzania, imetupilia mbali kesi ya kugombea nyumba namba 140 iliyopo eneo la Sekei Arusha baina ya makamishna wawili wa Jeshi la Polisi, Godfrey Nzowa, ambaye ni Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Aidha, mahakama hiyo imeamuru Nzowa kulipa gharama. Akisoma jana maamuzi ya Mahakama yaliyotolewa na majaji watatu wa vikao vya mahakama ya rufaa vinavyoendelea Jijini Arusha, ambao ni Mwenyekiti wa jopo la kikao cha mahakama ya rufaa, Jaji Mbarouk Salum Mbarouk, Mussa Kipenga na Bernad Luanda, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Elizabeth Mkwizu, alisema kesi hiyo imeondolewa katika usikilizwaji wa vikao vya mahakama hiyo kwa sababu za kiufundi. “Sababu ya kuondoa kesi hii ni mkata rufaa Nzowa… alichelewa kukata rufaa ndani ya siku 60 na hivyo kuwa nje ya sheria kama inavyotakiwa, ukitaka kukata rufaa, ukate rufaa ndani ya siku 60 tangu kesi ya msingi ku...