Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Asema Hakuna UGAIDI Jijini Humo.......Adai Mauji Msikitini ni Tukio ya Uhalifu wa Kawaida Kama Yalivyo Mengine
Wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza likiwashikilia watu 14 kwa tuhuma za mauaji ya watu watatu katika Msikiti wa Rahman uliopo Ibanda, Kata ya Mkolani mjini Mwanza, Mkuu wa mkoa huo, John Mongella amesema mauaji hayo hayana sura ya ugaidi. Mongella amesema mauaji hayo hayafanani na vitendo vya aina hiyo, hivyo ni vigumu kuyahusisha na ugaidi bali ni uhalifu kama ulivyo mwingine. Bila kufafanua, alisema mauaji mengine yanasababishwa na ndugu na jamaa za marehemu. Kadhalika, aliwataka viongozi wa mtaa huo kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi vitakavyoweza kukabiliana na uhalifu wa aina hiyo. Mauaji hayo yalitokea Mei 18, saa mbili usiku wakati waumini hao wakiwa msikitini wanaswali. Waliouawa katika tukio hilo ni Imamu wa msikiti huo, Feruz Ismail, Mbwana Rajabu na Khamis Mponda, wakazi wa Ibanda na kumjeruhi Ismail Ghati. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika msako dhid ya wahalifu unaoendelea maeneo mbalimbali mkoani humo....