NINI ESPERANÇA HATA WANGELETWA MAZEMBE, YANGA HII INAENDA HATUA YA MAKUNDI!!
Na Eusebius Paul Mara ya mwisho kwa club ya Tanzania kufuzu hatua ya makundi ya michuano barani Africa ilikuwa mnamo mwaka 2003! Kipindi ambacho serikali ya awamu ya tatu ilikuwa chini ya utawala wa Benjamin ‘Che’ Mkapa, Daz Nundaz na hit song ya Kamanda ndiyo uliikuwa ‘wimbo wa taifa’ wakati huo; CR7 alikuwa bado anakimbiakimbia kwenye nyasi za Estádio José Alvalade akiwa na jezi Sporting Lisbon. Kikosi kilichowajumisha wataalamu Juma Kaseja, Victor Costa Nampoka ‘Nyumba’, Boniface Pawasa, Mrundi Ramadhan Wasso, Christopher Alex ‘Masai’ (R.I.P), Selemani Matola (captain), Shekhan Rashid, Ulimboka Mwakingwe ‘Uli’, Yusuph Macho ‘Musso’, Emmanuel Gabriel ‘Batistuta’, Joseph Kaniki ‘Golota’ na Steven Mapunda ‘Garrincha’ chini ya benchi la marehemu James Aggrey Siang’a kiliwashtua wengi barani Africa. Kipindi hicho mwandishi wa makala hii nikiwa darasa la 5B ...