CCM MKOA WA ARUSHA YAMCHAGUA LEKULE KUWA MWENYEKITI ,HUKU SHABANI MDOE AKIIBUKA KATIBU MWENEZI
CHAMA cha Mapinduzi ( CCM)mkoa wa arusha kimefanya uchaguzi wa mwenyekiti wa mkoa na kufanikiwa kumchagua Maiko Lekule aliyepata kura 515 dhidi ya mgombea mwenza Emanuel Makongoro aliyepata kura 338,huku katibu mwenezi wa chama hicho akichaguliwa kuwa ni Shabani Mdoe aliyeshinda na fasi hiyo kwa kupata kura 36. Aidha katika uchaguzi huo wa mwenyekiti wajumbe halisi waliopaswa kuhudhuria ni 960 ambapo waliohudhuria ni 903 huku wajumbe halisi waliopiga kura wakiwa ni 861. Akitangaza matokeo hayo jana msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm taifa Stephen Wassira alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa huru na amani na hivyo ana imani kuwa uongozi huo utakiletea mabadiliko makubwa chama cha mapindizi katika mkoa huo. Alisema kuwa katika mkoa wa arusha matatizo ya umoja na tofauti yapo na kwamba atakayemaliza mzizi huo ni mwenyekiti aliyepatikana kwa kuhakikisha kuwa anawaunganisha wana ccm ili wawe kitu kimoja. “h...