Familia za Watu 8 Waliouawa Kwa Kuchinjwa Tanga Kujengewa Nyumba
Wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Tanga wameahidi kujenga nyumba nne kwa ajili ya makazi ya kaya ambazo ndugu zao waliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana katika kitongoji cha Kibatini, Jumanne ya wiki iliyopita. Wakazi hao walihamia katika eneo la Kona Z baada ya ndugu zao wanane kuchinjwa na watu hao katika tukio linaloonekana kama kulipiza kisasi baada ya wakazi hao kuwaripoti polisi watoto wanane walioonekana kwenye kitongoji chao na kutiliwa shaka. Wabunge waliahidi kujenga nyumba hizo baada ya kukuta familia hizo zikiishi katika mazingira magumu kwenye makazi yao mapya huku vyombo vyao vikihifadhiwa uwanjani. Walitoa ahadi hiyo jana walipokwenda kutoa rambirambi kwa familia hizo. Wabunge hao wote wakiwa wa CCM ni Adadi Rajabu wa Muheza, Jumaa Awesso na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. “Hii haiwezekani, binadamu hawezi kuishi katika mazingira kama haya, hawa wananchi wapo katika machungu ya kufiwa, inatia simanzi kuona wamehami...