Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wenje kuita mashahidi 700

Wenje kuita mashahidi 700

Picha
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje  Kahama/Mwanza. Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje (pichani) anakusudia kuita mahakamani zaidi ya mashahidi 693 kupinga ushindi wa mbunge wa sasa, Stanslaus Mabula (CCM). Wakili wa Wenje, Deya Outa aliieleza mahakama kuwa mashahidi hao ni pamoja na waliokuwa wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura, wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana. “Tunatarajia kuita mahakamani mashahidi wasiopungua 693 kuthibitisha madai yetu, kulingana na mahitaji ya hoja tunazotaka kuzithibitisha mahakamani,” alidai wakili Outa. Pande zinazohusika kwenye shauri hilo namba 3 la mwaka 2015, juzi ziliweka wazi hoja wanazokubaliana na zile wanazobishania kabla ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Kakusulo Sambo anayesikiliza shauri hilo kuihairisha hadi Machi 14, mwaka huu, itakapoanza kusikilizwa mfululizo. Pamoja na Mabula, wadaiwa wengine katika shauri hilo linalov...