Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Pilikapilika za Israel kwa ajili ya kuanzisha vita vingine dhidi ya Gaza

Pilikapilika za Israel kwa ajili ya kuanzisha vita vingine dhidi ya Gaza

Katika kuendeleza siasa zake za kupenda vita katika Mashariki ya Kati, utawala wa Kizayuni wa Israel umo katika maandilizi ya kuanzisha vita vingine dhidi ya Ukanda wa Gaza.Moshe Yaalon, Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kuwa, utawala huo umo katika maandalizi ya kufanya shambulio jingine dhidi ya Ukanda wa Gaza huko Palestina. Moshe Yaalon ametoa vitisho hivyo dhidi ya Wapalestina akiwa katika meli ya kivita ya Marekani ya USS Carney ambayo kwa sasa ipo huko Haifa Palestina kwa ajili ya manuva ya kijeshi ya Israel na Marekani. Kushtadi vitisho vya viongozi wa Israel dhidi ya Wapalestina tena katika kipindi hiki ambacho utawala huo ghasibu unafanya luteka ya pamoja na Marekani ni jambo linaloonesha kuanza duru mpya ya pilikapilika za kijeshi za Israel katika Mashariki ya Kati ikishirikiana na Marekani, harakati ambazo zinaonesha kuendelea siasa za kupenda vita za utawala huo ghasibu. Vitisho vya Israel dhidi ya Gaza vinaendelea kutolewa katika hali ambayo, miaka ...