SWANSEA VS MAN CITY: MATCH PREVIEW
Uhasimu katika ya vigogo wawili wa jiji la Manchester yaani Manchester United na Manchester City leo unaweza kunoga zaidi kutokana na wawili hao kuwania kwa udi na uvumba nafasi ya kushiriki UEFA mwakani. Manchester City wana matumaini makubwa zaidi ya kuchukua nafasi hiyo endapo tu watafanikiwa kushinda mchezo wao dhidi ya wabishi Swansea City, mchezo utakaopigwa kunako dimba la Liberty (Liberty Stadium). Manchester United, ambao kwa sasa wako katika nafasi ya tano huku wakiwa pointi mbili nyuma ya Manchester City wanaomba majirani zao wapoteze huku wao wakishinda ili kuweza kupata nafasi hiyo. Swansea inawezekana ikawa klabu ya pili kuzifunga Chelsea, Liverpool, Manchester United na Manchester City (endapo wataifunga) katika uwanja wao wa nyumbani kwenye msimu mmoja, baada ya Blackburn kufanya hivyo mwaka 1993-94. Haya ni mambo manne ambayo unapaswa kufahamu kuelekea mchezo huo: Majeruhi na taarifa nyingine muhimu kutoka kila timu. Kwa mujibu wa mtandao wa T...