DPP Amng’ang’ania Zombe na Wenzake Wanne, Awachomoa Watano Baada ya Kubaini Ushahidi Alionao Hauwagusi
Mahakama ya Rufani jana ilianza kusikiliza rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na askari wenzake wanane kuhusu kesi ya mauaji waliyoshinda. Katika kesi hiyo namba 358 ya mwaka 2013, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anapinga Zombe na wenzake kuachiwa huru na Mahakama Kuu katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa ikiwakabili. Zombe na maofisa wenzake walifunguliwa mashtaka katika Mahakama Kuu wakidaiwa kuwaua watu wanne wakiwamo wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro, Januari 14, 2006. Mauaji hayo yalifanyika katika msitu wa Mabwepande, Dar es Salaam na waliouawa walikuwa Mathias Lunkombe, Sabinus Chigumbi maarufu kwa jina la Jongo pamoja na ndugu yake Ephrahim Chigumbi na dereva teksi, Juma Ndugu wa Manzese. Mahakama Kuu katika hukumu yake ya Agosti 17, 2009 iliwaachia huru washtakiwa wote baada ya kuwaona hawana hatia. DPP hakuridhika na hukumu hiyo na mwaka huohuo, alikata...