Huu ndiyo ukweli wa Kitwanga Kuhusu Ulabu
Stori: Mwandishi Wetu, WIKIENDA DAR ES SALAAM: Ajali ya kisiasa! Gumzo kuhusu Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ kumtumbua Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Muhangwa Kitwanga (56) kwa madai ya kuingia bungeni akiwa ‘amechangamka’ bado liko vinywani mwa Wabongo huku sasa, upande wa pili wa hali hiyo ukijulikana, Ijumaa Wikienda limechimba. Ijumaa iliyopita, JPM alitengua uteuzi wake akidaiwa kuingia mjengoni akiwa amelewa hivyo kukosa umakini wakati akijibu maswali ya wizara yake. Habari zilizonaswa na Wikienda zinasema Kitwanga ni mnywaji lakini si kwa kiwango cha kukosa umakini kiasi cha kushindwa kutiririka vyema kwenye kujibu maswali, ila siku hiyo ilisababishwa na msongo. MSIKIE HUYU “Mimi sikatai ndiyo, Kitwanga anapiga ulabu, lakini yule jamaa yuko makini sana. Huenda siku ile alizidisha lakini naijua sababu. “Unajua siku za hivi karibuni, jamaa amekuwa akiandamwa sana na baadhi ya wabunge kuhusu sakata la Kampuni ya Lugumi na ufungwaj...