Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mbowe Ataja Sababu 3 Zilizomfanya Awaongoze Wabunge wa UKAWA Kususa na Kutoka Nje Ya Ukumbi wa Bunge

Mbowe Ataja Sababu 3 Zilizomfanya Awaongoze Wabunge wa UKAWA Kususa na Kutoka Nje Ya Ukumbi wa Bunge

Picha
Kambi ya Upinzani bungeni jana imesusia kuwasilisha na kujadili hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, huku kiongozi wake, Freeman Mbowe akitoka nje ya ukumbi huo, akitaja kasoro tatu zilizosababisha wachukue uamuzi huo. Staili ya kususia kujadili hotuba hiyo ya bajeti ni mpya kwa kambi hiyo ya upinzani baada ya kutumia njia ya kutoka nje ya ukumbi wakati wa vikao vya Bunge la Katiba na baadaye kutumia njia ya kupiga kelele kukwamisha shughuli za chombo hicho wakati wa Bunge la Kumi. Jana, Mbowe aliwaambia waandishi nje ya ukumbi kuwa kasoro zilizofanya wachukue uamuzi huo ni kukiuka masuala ya kisheria katika utekelezaji wa bajeti, kutotangaza kwenye Gazeti la Serikali mabadiliko ya wizara na kutorushwa kwa vipindi vya Bunge kwenye televisheni. Mbowe, ambaye alikuwa akitarajiwa kusoma bajeti ya upinzani kuhusu Ofisi ya Waziri Mkuu, aliibuka na hoja hizo tatu kabla ya kuamua kutoka nje. “Bajeti inakuwapo kwa sababu ni hitaji la kisheria. Inapokuwa...