Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MREMBO PINKIETO:ASEMA DAIREKTA ALINIOMBA PENZI LANGU

MREMBO PINKIETO:ASEMA DAIREKTA ALINIOMBA PENZI LANGU

Picha
Gisela Joseph ‘Pinkieto’ Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo ya filamu, jina la Gisela Joseph ‘Pinkieto’ litakuwa si geni kwako. Huyu alikuwa ni sekretari wa marehemu Steven Kanumba lakini pia msanii aliyeigiza kwenye filamu mbalimbali. Wiki hii kupitia safu hii tunaye akijibu maswali 10 ambayo aliulizwa na Mwandishi Wetu Hamida Hassan. Unataka kujua ni maswali gani aliulizwa na akajibu vipi? Fuatilia mahojiano hapa chini… Ijumaa: Kifo cha Kanumba kimeathiri vipi maisha yako ya kisanii? Pinkieto: Kanumba alikuwa mtu muhimu sana kwangu, kufariki kwake nilihisi kama ndoto zangu zimezimika ghafla. Namshukuru Mungu alinipa nguvu ya kuendelea kupambana mpaka leo. Ijumaa: Ulipotoka kwa Kanumba ulienda kufanya kazi wapi? Pinkieto: Nilienda kufanya kazi kwa Masanja Mkandamizaji ambaye alinipa nafasi kama ileile (usekretari). Nikafanya pale kwa muda kisha baadaye nikaamua kujiajiri. Ijumaa: Umesema kwa sasa umejiajiri ni kazi gani unaifanya? Pinkieto: Nafany...