Jack Wolper Adaiwa Kutolewa vyombo nje na Mwenye Nyumba......
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ambaye hivi karibuni ameonekana kulegalega amedaiwa kutolewa vyombo vyake nje kwenye nyumba aliyokuwa amepanga maeneo ya Mikocheni jiji Dar. Chanzo chetu makini kabisa kinadaiwa kuwa kipindi staa huyo akiwa nchini Afrika Kusini aliwaacha ndugu zake kwenye nyumba hiyo lakini kwa kushindwa kulipia kodi kwa kipindi kinachotakiwa, kabla hata hajarejea mwenye nyumba aliamua kutoa vitu nje na ndugu wa staa huyo kila mmoja kuelekea anakokujua. “Maskini, wakati Wolper yupo Afrika Kusini aliwaacha ndugu zake kwenye nyumba hiyo lakini ilishindikana kulipa kodi hivyo mwenye nyumba aliwatimua ndugu zake,” kilisema chanzo hicho. Kilizidi kufunguka kuwa, baada ya Wolper kurejea nchini ilibidi kuishi hotelini mpaka sasa ili kukusanya fedha nyingine kwa ajili ya kupanga nyumba ambayo ataweza kuishi pamoja na ndugu zake. “Wolper na mpenzi wake tangu waliporejea nchini wanaishi hotelini, nafikiri wanajipanga ili waweze k...