Baada ya Omba Omba Kugoma Kurudi Kwao...Serikali Kutafuta njia Mbadala kwa Walemavu Ombaaomba
KUFUATIA agizo lililotolewa hivi karibuni na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam la kuondolewa ombaomba jijini humo, serikali inajipanga kutafuta njia mbadala ya kuwawezesha kiuchumi ombaomba ambao ni walemavu, anaandika Regina Mkonde. Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Abdallah Posi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu) amesema, siyo jambo sahihi kwa walemavu hao kuishi kwa kutegemea kuomba na kwamba, kitendo hicho kinakandamiza fikra zao za kutafuta njia mbadala ya kujikwamua kiuchumi. “Siyo sahihi kwa walemavu wanavyoishi kwa kutegemea kuombaomba kutokana na kwamba, kitendo hicho kinadumaza fikra zao na kusababisha hata wale wenye uwezo wa kujinyanyua kiuchumi kushindwa kufanya hivyo,” amesema Posi. Amesema, kati ya walemavu hao wapo baadhi yao wana ndugu na jamaa ambao wanauwezo wa kuwasaidia na kwamba, siyo wote ambao hawana mahala pa kuishi. “Hao walemavu wana ndugu na jamaa zao, se...