Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya DOCTOR WA MBEYA CITY AWATOA HOFU BENCHI LA UFUNDI

DOCTOR WA MBEYA CITY AWATOA HOFU BENCHI LA UFUNDI

Picha
KUELEKEA mchezo ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar, uliopangwa kuchezwa  tarehe 30 mwezi huu kwenye uwanja wa Manungu Complex uliopo Turiani mkoani Morogoro, Mkuu wa kitengo cha utabibu kwenye kikosi cha Mbeya City Fc, Dr Joshua Kaseko amesema   vijana wake wote wako tayari  kwa vita hiyo ya mwisho wa mwezi. Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema jioni ya leo wakati wa mazoezi ya kikosi hicho kwenye uwanja wa shule ya sekondari Igawilo, Dr Kaseko aliweka wazi kuwa urejeo wa mlinzi Deo Julius aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu umetia moyo licha ya matizamio ya siku kadhaa kabla ya kumkabidhi rasmi kwa kocha Kinnah Phiri kuendelea na program za mazoezi. Sina majeruhi kwenye kikosi changu, Deo Julius aliyekuwa kwenye majeruhi ya muda mrefu tayari anarudi kikosini, tuko kwenye matazamio ya mwisho kabla ya kumkabidhi kwa kocha mkuu kuendelea na program za mazoezi, tulipata pointi tatu mchezo uliopita baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo,...