Serikali Yaanzisha Mfumo Mpya Wa Malipo Ya Mishahara Kwa Watumishi Wa Umma
SERIKALI imeanzisha mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao. Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali katika wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu. Waziri Mkuu alisema mfumo huo ujulikanao kama LAWSON, unatumika kwenye ajira za watumishi wote nchini, wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa Waziri Mkuu alisema mfumo huo unasaidia kutunza, kutuma na kuhuisha taarifa za watumishi kwa wakati na kwa ufanisi tangu mtu anapoajiriwa hadi inapofikia wakati wa kupandishwa madaraja na hadi anapostaafu. Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, maafisa utumishi walipaswa kukusanya taarifa za watumishi wote walioajiriwa na kuzipeleka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili zikathibitishwe kabla ya kuzipeleka HAZINA kwa maandalizi ya mishahara. Akitolea mfano...