Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mambo Mawili Yanayoibana Serikali Katika Mgogoro wa Wanafunzi 7000 Waliotimuliwa UDOM

Mambo Mawili Yanayoibana Serikali Katika Mgogoro wa Wanafunzi 7000 Waliotimuliwa UDOM

Picha
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitilla Mkumbo amesema kuna mambo mawili yanayoibana Serikali katika mgogoro wa wanafunzi waliotimuliwa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom). Akizungumza jana kwenye kipindi cha ‘Kipima Joto’ kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV, Profesa Mkumbo alisema Serikali haiwezi kukwepa lawama, kwa sababu ndiyo iliyoanzisha utaratibu wa kudahili wanafunzi wa kidato cha nne kupitia mfumo maalumu kabla ya kuanza kusoma shahada ya chuo kikuu. Pia, alisema Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), haiwezi kuhusika moja kwa moja kwenye udhaifu uliojitokeza katika udahili wa wanafunzi hao, bali Seneti ya Udom inapaswa kuwajibika katika hilo. Alisema kuna udhaifu wa kiutendaji kwa seneti hiyo yenye mamlaka ya kudahili wanafunzi wenye sifa ambayo iliiacha kazi hiyo  mikononi mwa TCU. Mkumbo alisema kazi ya TCU ni kuidhinisha majina ya wanafunzi waliokwisha dahiliwa na chuo husika na si kuchagua. “Chuo chochote ndicho kinachagua...