Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya STARS ILIBIDI IFE 10-0

AFANDE SELE: KAMA SI UPENDO WA MAHREZ KWA SAMATTA, STARS ILIBIDI IFE 10-0

Picha
Mkongwe wa Bongo Flavor nchini Selemani Msindi maarufu kwa jina la Afande Sele amesema soccer ni miongoni mwa michezo yenye upendo wa hali ya juu huku akitoa sababu kadhaa katika kuthibitisha hilo. Afande Sele ameandika ujumbe kupitia account yake ya Instagram  ‘afandeseletz’ akielezea namna mchezo huo na watu wake walivyotawaliwa na upendo wa kweli kwa kuonesha matukio mawili yanayothibitisha hilo. Tukio la kwanza ni Daniel Alves kujitolea sehemu yake ya ini kumpa beki mwenzake Eric Abidal waliyecheza pamoja kwenye klabu ya FC Barcelona ambaye aligundulika kuwa na tatizo la ini na alihitaji apandikizwe kipande cha ini kutoka kwa mtu mwingine. Tukio la pili ambalo Afande Sele anaendelea kuonesha kuwa mchezo wa soka ulivyotawaliwa na upendo ni juu ya ile mechi ya marudiano kati ya Algeria vs Tanzania ambapo Tanzania ilipigwa goli 7-0 ugenini. Afande Sele anasema kama isingekuwa Samatta kuhurumiwa na Riyad Mahrez (mchezaji wa timu ya taifa ya Algeria na klabu ya Leicester City ya...