𝗞𝗜𝗦𝗢𝗠𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗔𝗥𝗨𝗕𝗔𝗜𝗡𝗜 𝗕𝗔𝗔𝗗𝗔 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗜𝗧𝗜 𝗞𝗨𝗙𝗔 𝗡𝗜 𝗦𝗨𝗡𝗡𝗔𝗛 𝗔𝗨 𝗕𝗜𝗗𝗔𝗔?
SWALI: Imezoeleka maiti anapozikwa baada ya siku tatu watu hufanya kisomo, wengine hufanya Arobaini je hiki kisomo haswa kinahitajika kifanyike lini? na hii Arobaini inabidi iwe imesomwa kabla au baada ya kupita siku Arobaini tangu kupita mazishi? JIBU: AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu, Swalah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho Hakika ni kuwa jambo hili la kufanya kisomo baada ya siku tatu au kufanya arobaini na watu kula mpunga kama katika karamu ni mambo yaliyozoeleka sana. Zipo sehemu nyingine wanakusanyikana Msikitini kwa ajili ya kisomo kwa siku tatu mfululizo. Lakini kwa kuwa uchumi umezorota huwa siku hizi inafanywa siku moja peke yake na thawabu ya kisomo wanaona zinamfikia maiti. Hakika jambo hili halikuthubutu kabisa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi w...