Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Serikali yahamasisha wawekezaji viwanda vya kuongeza thamani

Serikali yahamasisha wawekezaji viwanda vya kuongeza thamani

Picha
Serikali imewataka wawekezaji wa ndani na nje kutumia fursa zilizopo Tanzania hasa katika eneo la kuongeza thamani ya malighafi mbalimbali. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru alipokuwa akiongea na maafisa kutoka kampuni ya nchini Ufaransa ya Endel Engie mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Maafisa wa kampuni hiyo walikuwa nchini na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali waandamizi wa serikali kueleza nia yao ya kuwekeza Tanzania na kujua fursa zilizopo nchini. Endel ni moja ya makampuni ya Engie Group yenye mapato yanayofikia Euro milioni 700 kwa mwaka na waajiriwa 6,000 nchini Ufaransa. Baadhi ya shughuli za kampuni hiyo ni katika maeneo ya sayansi za anga, viwanda vya vyakula, reli, gesi, ujenzi wa meli, nishati ya nyuklia na viwanda vya chuma miongoni mwa vingine. Kwa bara la Afrika, kampuni hiyo inafanya kazi katika nchi za Afrika ya Kusini, Angola na Congo DRC. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mk...