Aibu, Fedheha ya Mabasi ya Mwendo Kasi, Jiji, Manispaa Dar
IKIWA ni siku tano kupita baada ya mabasi ya mwendo kasi kuanza kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam, hali ya vituo vyake inatisha, anaandika Happiness Lidwino. Baadhi ya vituo hivyo vinatoa harufu kali, vimeenea mikojo, kinyesi na takataka ngumu ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na manispaa husika vimedai kutohusika na usafi wake. Miongoni mwa vituo alivyotembelea mwandishi wa habari hii ni pamoja na Moroco (Kinondoni), Kinondoni B, Manyanya na Kimara Baruti ambapo vituo hivyo vimekuwa na hali inayotia shaka usalama wa abiria wanaotumia vituo hivyo kusubiri usafiri. Gatson Makwembe, Msemaji wa Jiji alipoulizwa kuhusu ufuatiliaji wa usafi kwenye vituo hivyo baada ya hali kuwa mbaya, amedai jiji halihusiki. “Mimi siwezi kuzungumzia suala hilo kwani sisi halituhusu labda uwatafute Dart au Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni,” amesema Makwembe. Sebastian Mhowera, Ofisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni alipou...