Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya FAIDA ZA PARACHICHI

FAIDA ZA PARACHICHI

Picha
Parachichi ni tunda ambalo mti wake hujulikana kisayansi kama Persea amerikana.  Tunda hili lina aminika kuwa na asili kutoka jimbo la Puebla, bara Amerika ya kusini kunako nchi ya Mexico. Ushahidi wa kale kabisa, takribani miaka 10000 BC umeonyesha parachichi lilitumika katika jimbo la Puebla nchini Mexico. Lakini kutokana na faida nyingi kiafya zipatikanazo kwa ulaji wa tunda hili, tunda hili sasa hupatikana na kutumika kwa lishe sehemu nyingi duniani hususani barani Afrika. Parachichi ni tunda la pekee ukilinganisha na matunda mengine, kimsingi matunda mengine huwa yana wanga(carbohydrate) kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya. Jedwali likionyesha kiasi cha virutubisho katika gramu 100 za parachichi. Aina ya kirutubisho Kirutubisho Kiwango kilichopo Vitamini Vitamini A 7ug Vitamini E 2.1ug Vitamini C 10mg Thiamine 0.1mg Niacini 1.7mg Vitamini B 6 0.3mg Folic acid 81ug Madini Kalshamu 12mg Phosphorasi 52mg Magnesia...