Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya FUATA UTARATIBU HUU

MAKALA YA SHERIA: JE UNAHITAJI KUPIMIWA ARDHI MJINI, FUATA UTARATIBU HUU

Na  Bashir  Yakub. Tunapoongelea  upimaji   ifahamike  kuwa  upimaji  upo  wa  aina  nyingi.Kutokana na hilo upimaji  unaoongelewa  hapa  ni  upimaji  miliki. Lakini  pia  tunaongelea   upimaji miliki wa  ardhi  mijini na  sio vijijini. Upimaji wa  ardhi miliki ni  upimaji  ambao  lengo  lake  ni  kummilikisha  mtu  ardhi.  Kummilikisha  mtu  ardhi  sio  kumuuzia  ardhi.  Kummilikisha  mtu  ardhi  ni  kutambua  ardhi  yake  kimipaka  na  kumpatia  nyaraka  mahsusi(specific)  inayohusiana  na  umiliki( hati).   Kwa  maana  hii  wanaomiliki  ardhi  ambazo  hazijapimwa   hatuwezi  kusema  wamemilikishwa  ardhi . Haijalishi  ardhi  hizo  ni  za  kwao na ...